MOVE WITH MOVERS YOUTH CAMP :GROWING IN THE KNOWLEDGE OF GOD THROUGH CHRIST, KWANINI TUJIFUNZE KUHUSU YESU KATIKA KUMJUA MUNGU?: na APOSTLE SHEMEJI MELAYEKI.
Why Jesus should be a
complete prototype to know GOD?
Yohana 1:1-5
“Hapo mwanzo
kulikuwapo Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa na Mungu.
Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo, wala pasipo yeye
hakikufanyika chochote kilichofanyika”
Yohana 1:14
“Naye Neno alifanyika
Mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee
atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli”
“Ukimuona Yesu
umemuona Mungu katika mwili wa damu na nyama”
Jesus means God in Flesh.
Huwezi kumfunua Mungu
katika mwili kwa akili za damu na nyama.
Yohana 1:16-17
“Kwa kuwa katika
utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. Kwa kuwa torati ilitolewa kwa
mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu”
Kuna tofauti ya GOD
WITH US na GOD IN US. God with us waliexperience Wanafunzi wa Yesu walioishi naye katika hali ya mwili.
Mungu ndani yetu ina
nguvu zaidi kuliko Mungu pamoja nasi. [God in us is so powerful than God with
us]
Kabla Yesu hajafa
hakukuwa na mtu aliyekuwa na Mungu ndani yake. Yesu alipofufuka hakuitwa tena
Mwana wa Pekee wa Mungu bali alikuwa Mzariwa wa kwanza kati ya ndugu wengi.
“Mtu ambaye hawezi kuamini Mungu
alikuja katika mwili, hawezi kuamini kuwa Mungu anaweza kukaa ndani yake.”
Kwanini Yesu kumdhihirisha Mungu?
1.
HAKUNA ALIYEWAHI KUMWONA MUNGU
Yohana 1:18 “Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote;
Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye Aliyemfunua”
Yesu alipofufuka
alikwenda na mwili aliofufuka nao. Yesu alikwenda mbinguni na mwili wake.
Ukitaka kujifunza kuhusu Baba (Mungu) mwangalie Yesu kama PROTOTYPE ya Baba.
Muda wote ambao Yesu
alikuwepo alikuwa aki-demonstrate Namna Mungu alivyo.
Jesus is the Father
Manifestated. Hakuna anayeweza
kumwelezea Baba kama Yesu Kristo.
God came back to our level to help us not to be like us. That is why when
Jesus met with People he changed their Life.
Kabla ya kwenda Msalabani; Yesu hakuwa na biashara nyingine
zaidi ya kumfunua MUNGU
Yohana 4:34 “Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake ”.
Chochote ambacho Yesu alikifanya kilikuwa ni mapenzi ya
Mungu kwa wakati huo.
Yohana 5:24 “Amin,
amin nawaambia, Yeye alisikiaye Neno
langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii
hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani”
Yohana 5:30 “Mimi
siwezi kufanya neno mwenyewe kama nisikiavyo
ndivyo nihukumuvyo…”
Yohana 14:10-12 “Husadiki
ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno
niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu, lakini Baba akaaye ndani yangu
huzifanya kazi zake. Mnisadiki ya kwamba mimi na ndani ya Baba, na Baba yu
ndani yangu; la Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe. Amin
amin, nawaambieni, yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye
atazifanya; naam na kubwa kuliko hizo…”
Yohana 14:8-9 “Filipo
akamwambia, Bwana, utuoneshe BABA yatutosha. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwepo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe
usinijue Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuoneshe Baba”
Mathayo 17:1-5| Marko
1:10-11
Mifano ya Utimilifu wa Torati kuwa na maana.
Sabatho kuwa
Yesu[Pumziko]
Eneo la kuabudia [Kwa
mwanamke Msamaria-: Yoh 4:23]
Eliya na Musa ni kama
watu waliokuwa wanakabidhi Nyaraka kwa Yesu. Musa pia alitabiri habari za Yesu
Kumbukumbu 18:15
“Bwana, Mungu wako atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi. Msikilizeni yeye”
Mathayo 11:29
MUSA NA ELIYA
HAWAKUWAHI KUMWONA?
Kutoka 33:18 “Akasema,
nakusihi unionyeshe utukufu wako”
Kutoka 33:20 “Kisha
akasema, Huwezi kuniona uso wangu maana mwandamu hataniona akaishi”
Kutoka 33:21-23 “Bwana
akasema, Tazama, hapa pana mahali karibu name nawe utasimama juu ya mwamba…”
2 Wafalme 19:11-13
VITU AMBAVYO YESU
ALIVYOVIBADALISHA TUKITEGEMEA AFANYE KAMA MUSA NA ELIYA LAKINI HAKUFANYA
1.
Kushusha Moto; Luka 9:51-56 “…Wanafunzi wake Yakobo na
Yohana walipoona hayo walisema, Bwana, wataka tuangamize moto ushuke kutoka
mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya?]. Akawageukia
akawakanya. [Akasema hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo].
Kwa maana mwana Adamu hakuja kuzingamiza roho za watu, bali kuziokoa,
Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine”
Ukielewa Mungu anvyofanya kazi ni rahisi sana kufanya naye
kazi. Jambo kubwa tunalojifunza hapa ni kuwa Wanafunzi wa Yesu walikuwa na Mazoea.
2.
Kupiga Mawe; Yohana 8:3-12 “…Basi katika torati Musa alituamuru
kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?. Nao
wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshataki. Lakini Yesu
akainama na kuandika…”
Walawi 20:10
Maana ya maneno ya Yesu yalikuwa na maana kuwa “Huwezi kumhukumu mtu kwa sharia unayoivunja”
Approach ya Yesu
katika utatuzi wa matatizo ilikuwa inayosukumwa na UPENDO na sio Sheria.
3.
Mungu kumsikia mwenyewe Dhambi.
Dhana iliyokuwa imejengeka katika mioyo ya watu ilikuwa ni
kuwa Mungu
hasikii wenye dhambi
Luka 18:9-14
“Kutumia matendo yako kudai haki mbele za Mungu ni kuukosea
utakatifu wa Mungu na kazi ya Msalaba; maana Hakuna hata mmoja anayweza
kuihesabia Haki mbele za Mungu na akaonekana ana haki kwa 100%. Mungu anatoa
haki bure kwa kumwamini Yesu Kristo hasa kwa sababu ya kazi alizofanya ili sisi
tuhesabiwe haki”
Kama Mungu hamsikilizi mwenye dhambi, Mungu anamsikiaje mwenye
dhambi anapotubu?
Tunaposema Mungu
haongei na wenye dhambi, Mungu aliongeaje na
1.
Adamu: Mwanzo 3:9 “Bwana Mungu akamwita Adamu akamwambia Uko Wapi?”
“Watu wanajikweza
kwenye maisha, wanajishusha kwenye maombi”
2.
KAINI: Mwanzo 4:9 “Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili
ndugu yako? Akasema, sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”
Mwanzo 4:15-17 “Bwana akamwambia,
kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba, Bwana
akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga. Kaini akatoka mbele za uso wa
Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni. Kaini akamjua mkewe; naye
akapata mimba akamzaa Henoko; akajenga mji akauita HENOKO Kwa jina la mwanawe”
Mathayo 23:15
Hakuna maoni: