MAMBO YA MSINGI KUYAJUA NA KUYAFANYIA KAZI KUHUSU AGANO LA KALE NA AGANO JIPYA KATIKA KIZAZI HIKI
1. Agano la kale liliishia au lilifungwa na Yohana Mbatizaji kimsingi, ila kwenye mpangilio wa vitabu aliwekwa Malaki.
Mathayo 11:13
Luka 16:16.
2. Agano jipya lilianzishwa na kusimamiwa na Yesu mwenyewe, nalo linahubiri habari njema ya Ufalme wa Mungu.
Mathayo 4:17
3. Agano la kale limefungwa ndani na katika sheria, agano jipya ni udhihirisho wa neema ya Mungu kwa wanadamu wote.
Tito 2:11
4. Agano la kale ni namna ambavyo Mungu alitembea na mwanadamu nyakati hizo, kuna namna Mungu alijifunua na kujidhihirisha zamani tu.
5. Agano la kale ni kuukuu, limechakaa na lilitoweka pindi agano jipya lilipoanza.
Waebrania 8:13
6. Agano la kale lilikuwa na mapungufu, lilihitaji kujazilizwa au kufanywa kamili, kama lingekuwa limekamilika basi kusingekuwa na haja ya kuja kwa agano jipya.
Waebrania 8:7
7. Ndani ya agano jipya, Kuhani Mkuu ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba, ila katika agano la kale kuhani mkuu alikuwa anaishi katikati ya wanadamu siku zote za maisha yake.
Waebrania 8:1-5
8. Kwenye agano la kale, sadaka za wanyama kama mbuzi na kondoo ndio walikuwa wanatumika ili kuwafutia dhambi wakosaji mara moja moja kila wanapokosea. Kwenye agano jipya ni damu ya Bwana Yesu mwenyewe ndio inayofuta dhambi na ni mara moja tu.
Waebrania 9:14
9. Mahukani wote wa agano la kale walikufa moja kwa moja mpaka watakapofufuliwa tena na Kuhani Mkuu wa agano jipya aliye kufa na kufufuka kama alivyotangulia kusema.
10. Makuhani wa agano la kale wote walitoka katika kabila la LAWI, ndo ukisoma kitabu cha MAMBO YA WALAWI ila Kuhani Mkuu wa agano jipya yeye alitoka Kabila la Yuda.
Waebrania 7:14
11. Ndio maana Kuhani Mkuu wa agano jipya alifanikiwa kumnunulia Mungu watu kutoka kila kabila, lugha na jamaa ili wawe vipawa na karama zake za milele.
Ufunuo 5:9-10
12. Kuhani akibadilika lazima na sheria zibadilike.
Waebrania 7:12.
Kama makuhani wa agano la Kale walibadilika na nafasi yao wote ikachukuliwa na Kuhani Mkuu mpya yaani Bwana Yesu, basi ni lazima kuishi katika upya wa sheria za Kuhani mwenyewe, yaani AGANO JIPYA LA NEEMA
13. Yesu kama Kuhani Mkuu wa Agano bora zaidi na lenye ahadi bora zaidi, aliinua VIWANGO VYA KIMUNGU katika namna ambayo hakuna mwanadamu anaweza KUMPENDEZA MUNGU bila kusaidiwa na Bwana Yesu mwenyewe.
14. Agano jipya lina viwango vya juu zaidi kuliko agano la kale, neema ina nguvu zaidi kuliko sheria, sheria inaumiza mwili, neema inaponya. Bwana Yesu alihamisha sheria toka mwilini mpaka moyoni na ndio maana kuishi ndani ya neema ya Mungu ni kazi ngumu zaidi kama ukitumia sheria.
15. Agano la Kale lilikuwa na sheria nyingi ambazo hakuna mwanadamu alifanikiwa kuzifikia ndio maana Bwana Yesu alikuja kuleta neema ili kuifanya sheria ipate maana yake ndani ya neema ya Mungu. Kwenye Agano Jipya, sio lazima ufumaniwe ndo uwe na hatia bali hata ukitamani mawazoni mwako tayari uko hatiani.
16. Kama Agano la Kale lingekuwa limejitosheleza, kusingekuwa na Agano Jipya.
17. Kama kabila la Lawi tu ndo lingetakiwa kutoa Makuhani hata kwenye agano jipya, Yesu asingekuwa kuhani Mkuu tokea kabila la Yuda.
18. Kama sheria ingetosheleza, neema isingehitajika kabisa.
19. KAKA YAKE MWANA MPOTEVU ALIKUWA MTUMWA ZAIDI YA MWANA MPOTEVU MWENYEWE. JICHAGULIE UPANDE.
NITAENDELEA.
RAPHAEL LYELA
0744644699.
Mtumishi umeelezea vizuri agano jipya na la kale je? Mathayo 5:17 unaelewaje
JibuFuta