Ads Top

NANI ANAKUDUMAZA, KAMA HAUJAJIDUMAZA MWENYEWE.



Kuna watu wakikusogelea tu unaanza kurudi nyuma katika hatua za mipango yako. Kuna watu wakija karibu na wewe tu unaanza kuwa maarufu katika kutenda dhambi na kuishi Maisha ya uovu. Kuna mtu akiwa Rafiki yako anakusimamisha, yaani unakuwa huoni hatua yoyote unayopiga kwenda mbele. Kuna watu walipokuja karibu nasi tu basi hali ya KUDUMAA ikaanza kuchukua nafasi yake. Unabaki unatingishika tu bali hakuna hatua unapiga. Unabaki unayumbayumba lakini huanguki kabisa wala husimami kabisa. Nani anakudumaza? Wengine wamedumazwa na mitandao ya kijamii, wengine wamedumazwa na nini sijui huko. Ukidumaa maana yake huwezi kukua, kuendelea, kusitawi wala kupiga hatua.

Ukijiangalia unajionaje, umedumazwa au umejidumaza? HONGERA KWA VYOTE.
Classified Mindset
RAPHAEL LYELA

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.