HEKIMA ZA NDEGE
Wako aina mbali mbali za ndege. Ndege wako wa aina mbali mbali duniani. Ndege hawa, japo kwamba wote ni ndege lakini hawaruki pamoja, hawali pamoja, hawalali pamoja au maeneo yanayofanana. Hakuna ndege anaemuiga mwingine kuruka au kulia au kula. Kila ndege katika upekee wake anatafuta wale wanaofanana. Ndio maana ule msemo ukasema, ndege wenye mabawa huruka pamoja na kila ndege ana mabawa. Ukiwaona ndege wako kwenye kundi ujue wote ni jamii ya ndege wanaofanana na wako kwenye ukoo huo. Ndio maana Tai haruki na Njiwa, ingawa wote ni ndege. Kuwa tofauti sio dhambi, kikubwa ni kujitambua kuwa wewe ni wa tofauti kwakuwa ni wa pekee. Upekee wetu ni ladha muhimu sana, tunahitajiana na kwa jinsi hii MUNGU HUTUFIDIA katika mapungufu yetu. Jifunze kwa ndege ili usijikute unataka kufanana na kila mtu, unataka kuiga kila kitu. Kanuni ya hekima, UKITEMBEA NA MWENYE HEKIMA ATAKUAMBUKIZA HEKIMA. Sasa nikuulize swali kimsingi, NI VIGUMU KWAKO KUJIFUNZA HEKIMA YA NDEGE?
Rafiki wa Seremala
Pastor Raphael Lyela
0744644699.
Hakuna maoni: